Mkufunzi wa chuo kikuu cha Alqadisiyya Dokta Fadhili Kitabu Dahashi amesema kuwa, chuo kikuu cha Al-Ameed kimekuwa mstari wa mbele daima katika kusaidia watafiti na wabobezi.
Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya maonyesho ya ubunifu kwa mnasaba wa maadhimisho ya wiki ya fikra za kibunifu, chini ya kauli mbiu isemayo “Ubunifu na malengo ya maendeleo endelevu katika kujenga mustaqbali shirikishi”.
Akasema kuwa “Washiriki wa maonyesho haya wameonyesha kinga iliyotengenezwa kwa vitu vya asili, inayosaidia kuzuwia kuathirika kwa mimba kutokana na mionzi ya (x-ray)”.
Katika maonyesho hayo, wameshiriki watafiti na wabobezi kutoka vyuo vikuu na taasisi tofauti, bunifu mbalimbali zinazohusu mambo tofauti zimeonyeshwa sambamba na kuhimiza kuendelea kufanya tafiti na ubunifu katika mambo mbalimbali.