Kikosi cha Abbasi (a.s) kinafanya maonyesho ya ushindi wake katika kitongoji cha Bashiru mkoani Kirkuuk.

Kikosi cha Abbasi (a.s) kimefanya maonyesho ya ushindi wake dhidi ya magaidi wa Daesh katika kitongoji cha Bashiru mkoani Kirkuuk.

Maonyesho yameratibiwa pembezoni mwa kongamano la kumbukumbu ya mwaka wa nane toka kukombolewa kwa kitongoji cha Bashiru, chini ya kauli mbiu isemayo (Ukombozi wa Bashiru.. tukio la pekee katika ubao mtukufu), yanasimamiwa na kikosi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa lengo la kuwakumbuka mashahidi wa ukombozi wa kitongoji cha Bashiru dhidi ya makaidi wa Daesh.

Maonyesho hayo yanahusisha siraha zilizotekwa na wapiganaji wa kikosi kutoka kwa magaidi wakati wa mapambano katika mji huo, maonyesho yamepambwa kwa siraha nzito, za kati na nyepesi, pamoja na ndege zisizokua na rubani, siraha nyeupe na mapanga, bila kusahau vifaa vya mashahidi wa kikosi, kama vile mavazi, siraha na baadhi ya vitu vyao binafsi.

Sayyid Abbasi Yasini Mahmuud mmoja wa wakazi wa mji huo amesema “Maonyesho ya kikosi cha Abbasi (a.s) yanalenga kudumisha kumbukumbu za mashahidi wa kikosi cha Abbasi na askari walioshiriki katika kukomboa kitongoji cha Bashiru”.

Akaongeza kuwa “Vifaa vilivyo onyeshwa kuanzia mfuko wa hela, picha na vifaa vya kivita vinatufanya tujihisi kukutana na mashahidi wetu daima na kuadhimisha damu zao takatifu zilizokomboa mji wa Bashiru”.

Maonyesho yamepata muitikio mkubwa kutoka kwa wakazi wa mji huo, ambao wamepongeza maonyesho haya yanayo onyesha tukio muhimu kihistoria katika vita dhidi ya magaidi iliyo ongozwa na kikosi cha Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: