Kuwapa zawadi familia za mashahidi katika kumbukizi ya mwaka wa nane toka kukombolewa kwa kitongoji cha Bashiru.

Miongoni mwa vipengele vya kumbukizi ya mwaka wa nane toka kukombolewa kwa kitongoji cha Bashiru katika mkoa wa Kirkuuk ni kutoa zawadi kwa familia za mashahidi.

Awamu ya nane ya kumbukizi ya kikosi cha Abbasi (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ukombozi wa Bashiru.. tukio la pekee katika ubao mtukufu).

Walio simamia ugawaji wa zawadi ni, muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Kirkuuk Sayyid Qambar Mussawi, kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Shekhe Maitham Zaidi, makamo rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Aadil Wakiil, Sayyid Hassan Mussawi, Shekhe Muntadhiru Aalu Musaafir, kamanda msaidizi wa polisi wa Kirkuuk Meja Jenerali Ali Mutwashar na Rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Askariyya Sayyid Muhammad Mussawi.

Utoaji wa zawadi unaonyesha namna Atabatu Abbasiyya inavyozijali familia za mashahidi, kama sehemu ya kuonyesha thamani ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kuilinda Iraq na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: