Idara ya maonyesho ya kimataifa katika mji wa Najafu: Atabatu Abbasiyya imethibitisha kusaidia uzalishaji wa ndani kwa kupaza kaulimbiu isemayo (Imetengenezwa Iraq).

Muongeaji rasmi wa maonyesho ya kimataifa mjini Najafu Sayyid Haidari Mussawi amesema kuwa Atabatu Abbasiyya imethibitisha kusaidia uzalishaji wa ndani kwa kupaza kauli mbiu isemayo (Imetengenezwa Iraq).

Ataba inashiriki kwenye maonyesho na kongamano la kibiashara awamu ya kumi na mbili mjini Najafu, kupitia shirika la Nurul-Kafeel na Khairul-Juud, jumla ya nchi nane za kiarabu na kiajemi zinashiriki kwenye maonyesho hayo, huku kukiwa na mashirika zaidi ya (200).

Mussawi amesema “Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho na kongamano la kibiashara katika mji wa Najafu, umethibitisha kuunga mkono na kusaidia kupaza kauli mbiu isemayo (Imetengenezwa Iraq)”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imepata mafanikio kupitia juhudi za wananchi wa Iraq, hivyo inafanya juhudi ya kusaidia uzalishaji wa ndani na kushiriki kwenye maonyesho kwa ajili ya kuingiza bidhaa katika mikono ya watumiaji kwa ujumla”.

Akabainisha kuwa “Tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi waliokuja kuangalia bidhaa zinazotengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: