Ataba imegawa chakula katika mji wa Diwaniyya

Atabatu Abbasiyya imegawa chakula kwa wahitaji katika kitongoji cha Afaku katika mji wa Diwaniyya.

Ugawaji huo umesimamiwa na kitengo cha Dini katika Ataba tukufu.

Sayyid Halim Kadhim amesema: “Kitengo kimegawa chakula kufuatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi kwa familia za masikini katika kitongoji cha Kafi wilayani Afaku”.

Akaongeza kuwa “Watu wa mji huo wanatatizo la upungufu wa maji safi ya kunywa na uhaba wa chakula, akasema kuwa ugawaji wa chakula utaendelea siku zijazo”.

Wakazi wa kitongoji cha Kafi wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa msaada huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: