Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba maalum ya wageni kutoka chuo kikuu cha Kufa.
Rais wa kitengo Sayyid Muhammad Ali Azhar amesema “Kitengo kimeandaa ratiba ya kitamaduni kwa wageni kutoka chuo kikuu cha Kufa, ratiba inahusisha kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutembelea makumbusho ya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Wageni wameangalia mali-kale zilizopo katika makumbusho na kusikiliza historia yake na namna zilivyo patikana na kuingizwa kwenye makumbusho hiyo”.
Akaendelea kusema “Ziara hiyo ni sehemu ya ratiba maalum ya kupokea wasomi na watafiti kutoka vyuo tofauti vya Iraq kwa lengo la kujenga ushirikiano baina ya vyuo vikuu na taasisi za kidini”.