Kamati ya program katika Atabatu Abbasiyya, imekamilisha shughuli za wiki ya nne katika mwezi wa pili mwaka wa pili wa mradi wa program za kila wiki kwa watumishi wa Ataba tukufu.
Program zinasimamiwa na kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, inavipengele vya kidini, kitamaduni, michezo, mafunzo maalum ya kujenga uwezo, mashindano tofauti pamoja na kutembelea miradi ya Ataba tukufu.
Ratiba inalenga kujenga ukaribu na mahusiano baina ya watumishi sambamba na kuwaonyesha harakati zinazofanywa na Ataba tukufu katika sekta ya viwanda, kilimo, malezi na utoaji wa huduma mbalimbali.
Kwa ajili ya kuwajenga kifikra na kiaqida, tuliweka ratiba ya kutembelea malalo ya Maimamu watakatifu.