Atabatu Abbasiyya imeweka mabango yanayo ashiria huzuni kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Kitengo kinachosimamia haram katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka mabango yanayoashiria huzuni katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).

Makamo rais wa kitengo kinacho simamia haram Sayyid Zainul-Aabidina Quraish amesema “Tumeweka mabango yanayo ashiria huzuni, sehemu zote za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumeweka mabango na vitambaa kwenye kuta na milango”.

Akaongeza kuwa “Mabango na vitambaa yamatengenezwa kwa vipimo maalum na kuwekwa kwenye maoneo tofauti ndani ya Ataba tukufu, huku mabango makubwa yakiwekwa kwenye kuta na milango”.

Akabainisha kuwa “Kazi hiyo hufanywa kwa utaratibu maalum bila kuathiri sehemu yeyote, mabango huwekwa kwa kutumia gundi maalum ambayo ni rahisi kutoa baada ya matumizi, mabango yanamaandishi na nakshi zinazoashiria huzuni, yamewekwa ndani ya haram tukufu hadi nje”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: