Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s) kwa kufanya Majlisi.

Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Kiongozi wa idara ya kupokea wageni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Farasi Husseini amesema “Ataba tukufu imefanya Majlisi ya kuomboleza katika ukumbi wa utawala ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi na mazuwaru”.

Akaongeza kuwa “Muhadhiri wa Majlisi Shekhe Hadi Karbalai ameongea kuhusu maisha ya Imamu Jafari Swadiq (a.s), mazingira ya kifo chake, ushujaa wake, ufasaha wake, kujitolea kwake katika kulinda uislamu na umuhimu wa kufuata mwenendo wake”.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum yenye vipengele tofauti katika kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: