Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani imefanya hafla ya wahitimu wake wa kwanza, waliosoma kwa muda wa miaka (6), miongoni mwa mada walizofundishwa ni (Nahau, Fiqhi, Aqida, Ulumul-Qur’ani, Balagha na hukumu za usomaji wa Qur’ani).
Akaongeza kuwa “Idara inazingatia na kutilia uhuminu sana harakati na miradi inayohusu Qur’ani tukufu”
Mwanafunzi Majidah Hussein Jaasim amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu kuandaa hafla ya wahitimu ni jambo zuri, hatuna la kusema zaidi ya kushukuru idara ya Ataba tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi na viongozi wa idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani kwa kazi kubwa waliyofanya ya kufanikisha ratiba hii”.