Atabatu Abbasiyya imefanya majlisiya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s).

Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Mahadi Farhani amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s) na kuhudhuriwa na watumishi wa Ataba tukufu na mazuwaru.

Akaongeza kuwa “Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imejikita katika kueleza Maisha ya Imamu Swadiq (a.s) na watawala wa zama zake”.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu yenye vipengele tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: