Kupitia maokibu ya pamoja.. wahudumu wa Ataba mbili wameomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s)

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.

Sayyid Budairi Mamitha kutoka idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya amesema “Maukibu imeanzia ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakisoma mashairi ya kuomboleza na yanayo bainisha msiba huo kwa waumini, wakaenda hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Maukibu ilipofika katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) ikafanya Majlisi ya kuomboleza ambapo zimesomwa qaswida na tenzi za kuomboleza zilizo elezea dhulma alizofanyiwa Imamu Jafari Swadiq (a.s)”.

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala hufanya maukibu ya pamoja katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: