Wanafunzi wa kike wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria wameanza kuwasiri kwenye ukumbi wa Jaamiatu-Zaharaa (a.s) katika wilaya ya Ainu-Tamru mkoani Karbala.
Hafla inasimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Hafla inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu) kwenye ukumbi wa Jaamiatu-Zaharaa katika kitongoji cha Ainu-Tamru, zaidi ya wanafunzi (300) kutoka shule tofauti wanashiriki.
Hafla itakuwa na vipengele mbalimbali, kama vile mawaidha, qaswida, mashairi, tenzi pamoja na kuimba wimbo wa ahadi ya kuwajibikiwa na sheria.