Wanafunzi wa shule za Ainu-Tamru wanaimba qaswida ya kuwajibikiwa na sheria.

Hafla ya wanafunzi wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria kundi la pili katika wilaya ya Ainu-Tamru mkoani Karbala kupitia mradi wa (Maua ya Fatwimiyya), imepambwa na qaswida ya kuwajibikiwa na sheria iliyo somwa na wanafunzi hao.

Hafla inasimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, kupitia mradi wa (Maua ya Fatwimiyya) awamu ya sita, chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu yangu inatokana na mwenendo wa Zaharaa na ufuasi wa Zainabu).

Hafla imehudhuriwa na viongozi wa Atabatu Abbasiyya, wazazi wa wanafunzi na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.

Zaidi ya wanafunzi wa kike (300) wameshiriki kwenye hafla hiyo wakiwa wamevalia vazi la Zainabiyya.

Hafla hiyo ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya katika kuandaa kizazi cha watu wanaoshikamana na mafundisho ya Dini tukufu ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: