Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa wito wa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kushikamana na Marjaiyya wa kidini.
Ameyasema hayo alipokutana na vijana wa muungano wa Imamu Hussein (a.s) kutoka mkoa wa Diwaniyya, akasikiliza maelezo kuhusu kazi za umoja huo na huduma za kijamii wanazotoa kwa wahitaji.
Katika maelezo yake Muheshimiwa Sayyid Swafi akasema, Hakika Maimamu watakatifu (a.s) wamehimiza kufuata amri zao na kuwa na mafungamano ya kudumu na wao, baada ya karne 14 kuna mafungamano ya wazi na Maimamu (a.s).
Sayyid Swafi akataja wanachuoni waliofariki (r.a) na waliopo hai, kwa namna wanavyo tunza turathi za Ahlulbait (a.s), jambo ambalo limerahisisha kurejea katika riwaha halisi na kutambua turathi zao.
Sayyid Swafi akasisitiza umuhimu wa kuwa chini ya Marjaiyya, kwani Maraajii na wanachuoni wanafanya kazi kubwa ya kuhifadhi vijana na familia na kuwalinda na misingi mibovu inayolenga kuharibu familia na jamii.
Akasema kuwa baadhi ya jamii zimetoka kwenye joho la Maimamu (a.s) na Imani, Pamoja na kuwa Ziaratu-Jaamia inasema, Hakika maneno yao (a.s) ni nuru, hayafai kuyatupa, au kuna mtu yeyote huilaani nuru.
Makamo katibu mkuu wa umoja huo Sayyid Qamaru bun Hashim Ahmadi Shaakir amesema “Tumesikiliza nasaha za Sayyid Swafi na umuhimu wa kufuata mwenendo sahihi kwa kuimarisha uhusiano na Ahlulbait (a.s) na kutambua historia halisi pamoja na kuimarisha uhusiano wetu na Imamu wa zama (a.f)”.
Akaendelea kusema “Tumemuambia Muhesimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kazi na huduma zinazotolewa na muungano wetu, ikiwemo kuhuisha maadhimisho ya Imamu Hussein, kutoa mihadhara mbalimbali, kufanya nadwa kwa wanafunzi wa vyuoni, kuhudumia mazuwaru, wagonjwa, mayatima, familia za mashahidi, kugawa chakula katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kugawa nguo wakati wa Iddi”.