Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi wapya.
Mkufunzi wa semina Sayyid Mustwafa Hakim amesema: “Semina imejikita katika kuwatambulisha watumishi wapya misingi ya maadili kazini na sifa wanazotakiwa kupambika nazo wakati wa kazi”.
Akaongeza kuwa “Wamesoma mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni maadili ya kiislamu na misingi yake, mbinu za kuamiliana na mazuwaru na namna ya kuamiliana na watumishi na idara zao”.
Akasema “Semina imefafanua misingi ya maadili mema, na namna ya kupambana na changamoto uwapo kazini pamoja na njia za kuwasiliana na kiidara”.