Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina yenye anuani isemayo (Uzuri wa kuandika kisa kifupi) kwa wasichana.
Mkufunzi wa semina hiyo ametoka chuo cha malezi katika mkoa wa Karbala Dokta Ammari Yasiri, ameongea maudhui tofauti, miongoni mwa maudhuo hizo ni uwelewa wa kisa na chanzo chake.
Semina inalenga kuwajengea uwezo wa mazingatio washiriki, na kuwashajihisha kuonyesha vipaji vyao katika uandishi wa visa vifupi katika jamii chini ya mwenendo wa Ahlulbait (a.s).
Semina inafanywa kwa muda wa siku tatu mfululizo kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu upande wa wasichana.