Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya vikao vya kuelezea historia ya Ahlulbait (a.s) katika mkoa wa Dhiqaar.
Vikao hivyo vimefanywa chini ya program ya mwanafunzi hodari inayo endeshwa na kituo cha Multaqal-Qamaru tawi la Dhiqaar chini ya kitengo, kwa lengo la kuimarisha uwelewa wa vijana.
Vikao vimeeleza historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kielimu na kidini, imeelezwa zaidi historia ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) kama mfano.
Vikao hivi ni sehemuya ratiba muhimu inayofanywa na kituo kwenye mikoa tofauti kwa lengo la kujenga uwezo wa vijana.