Mkuu wa mkoa wa Baghdad Muheshimiwa Abdulmutwalib Ali Al-Alawi amesema kuwa, Miradi ya Atabatu Abbasiyya iliyokamilika na ambayo bado inaendelea kutekelezwa, inaubora wa pekee.
Ameyasema hayo alipotembelea Ataba tukufu na kuangalia baadhi ya miradi ya Ataba, amesisitiza kuwa “Mashirika ya Atabatu Abbasiyya yanaendesha miradi bora zaidi kutokana na uzowefu mkubwa walionao katika kazi yao”.
Akaongeza kuwa “Miradi ya Atabatu Abbasiyya inaupekee wake katika ufanisi na ubora endelevu”.
Akasema kuwa, mkoa wa Baghdad utajitahidi kunufaika na uzowefu wa Atabatu Abbasiyya kwa kufanya kazi na mashirika ya Ataba katika mkoa huo, baada ya kuona mafanikio yao katika mkoa mingine.