Hafla imefanywa mbele ya mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Ataba Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, baadhi ya marais wa vitengo, viongozi wa idara na mazuwaru.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Ali Saaidi, ikafuatiwa na ujumbe kutoka uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya uliowasilishwa na Shekhe Ali Mujaani, ameongea kuhusu utukufu wa Bibi Fatuma Maasumah (a.s) na nafasi yake mbele ya Ahlulbait (a.s).
Kisha wahudhuriaji wakasikiliza qaswida na mashairi kutoka kwa Ridhwa Khafaji, Abu Muhammad Almayahi na Ghasani Quraishi huku tenzi zikisomwa na Sayyid Ibrahim Sharifi na Ali Anbari.
Hafla ikahitimishwa kwa kutangazwa majina ya washindi kumi wa shindano la kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatuma Maasuma (a.s) lililosimamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.