Mambo muhimu yaliyopo kwenye program ya mradi wa Khairaatu-Hisaan.

Program ya kwanza ya mradi wa (Khairaatu-Hisaan) iliyoratibiwa na maktaba ya Ummul-Banina ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya inavipengele tofauti.

Programa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na wimbo wa taifa kisha wimbo wa Lahnul-Iba na surat Fat-hah kwa ajili ya kurehemu mashahidi wa Iraq.

Halafu ukawasilishwa ujumbe kutoka ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, ulio wasilishwa na bibi Sara Halo.

Kiongozi wa idara ya maelekezo ya kidini bibi Adhraa Shaami ameongea kuhusu nafasi ya mwanamke kwa kuelezea kitabu cha (Ujumbe wa mwanamke katika Maisha) amebainisha maana ya kukamilika kimaadili.

Kikosi cha chemchem ya ubora kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya kimeshiriki kwa anuani ya (Abaa).

Bibi Sakina Khalili kutoka Lebanon akaongea kuhusu uzowefu wake katika swala la Abaa kupitia picha na vipande vya Video.

Bibi Rihabi Qazwini kutoka maktaba ya Ummul-Banina (a.s) akasimamia shindano la (Mirqaatul-Hisaan) ambalo lumehusisha makundi mawili ya wanafunzi, wameulizwa maswali na kupewa zawadi kundi lilipata pointi nyingi kushinda kundi lingine.

Shule ya Fadak Zaharaa (a.s) imeshiriki kusoma qaswida.

Mwisho wa hafla wanafunzi (250) wakiwa wamevaa Abaa ya Zainabiyya wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: