Majmaa-Ilmi imehitimisha semina ya kuwajengea uwezo mahafidhu katika mkoa wa Karbala.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha semina ya kuwajengea uwezo walimu wa kuhifadhisha Qur’ani katika mkoa wa Karbala.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Maahadi imekamilisha semina ya kuwajengea uwezo walimu wa mradi wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu”.

Akaongeza kuwa “Semina imedumu kwa muda wa mwezi mmoja, chini ya wakufunzi waliobobea katika fani za kuhifadhisha Qur’ani na ufundishaji, kwa lengo la kuwajengea uwezo walimu wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu”.

Maahadi inamradi wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine ya Iraq, zaidi ya wanafunzi (500) wanashiriki kwenye mradi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: