Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kinatembelea maktaba za mikoa ya kaskazini ya Iraq.
Ziara hiyo imesimamiwa na idara ya ufatiliaji katika ofisi ya Habari chini ya kitengo, imehusisha ugawaji wa machapisho ya kitengo kwenye vyuo vikuu vya serikali na binafsi na kwenye maktaba kuu za mikoa ya kaskazini.
Ziara imedumu kwa muda wa siku tano, wametembelea maktaba za vyuo na maktaba kuu katika miji ya (Nainawa, Dahuuk, Arbiil na Suleimaniyya).
Wamegawa zaidi ya machapisho mbalimbali (140), vitabu, majarida na kataloji zinazo elezea turathi za kiislamu katika Nyanja tofauti.