Balozi wa Saudia nchini Iraq Sayyid Abdul-Azizi Bun Khalidi Shimri, ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumatatu.
Muheshimiwa balozi amekutana na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na wajumbe wa kamati kuu, Sayyid Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Ali Azharu.
Amesikiliza maelezo ya huduma zinazotolewa kwa mazuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndaugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).