Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inaendelea na semina kwa lengo la kuhudumia vikundi vya Husseiniyya.

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na semina kuhusu upotoshaji wa vyombo vya Habari katika kuelezea huduma zinazotolewa na vikundi vya Husseiniyya.

Semina inafanywa kwa muda wa siku tano, washiriki wapo kumi kutoka mradi wa Fatuma Zaharaa (a.s) kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo ya Habari chini ya kitengo cha Habari, wanatoa mihadhara kuhusu upotoshaji wa vyombo vya Habari.

Idara imeandaa ratiba tofauti katika kuonyesho namna inavyo jali vijana wanaotoa huduma kwenye vikundi tofauti vya Husseiniyya, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kupambana na upotoshwaji wa maadhimisho ya Husseiniyya na madhehebu kwa ujumla.

Semina imeeleza kwa kina kuhusu upotoshaji unaofanywa na vyombo vya Habari, ukweli hubadilishwa kwa makusudi, au kuripoti jambo nusu na kutia shaka katika ukweli.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: