Ataba mbili tukufu Alawiyya na Abbasiyya zinajadili njia za kuimarisha ushirikiano katika kuhudumia mazuwaru watukufu.
Jambo hilo limefanyika wakati wa ziara ya rais wa kitengo cha kulinda nidhamu katika Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Karaar Hamza Aljamali pamoja na wajumbe aliofuatana nao katika Atabatu Abbasiyya, na kukutana na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Ali Muslihu.
Wamejadili kuhusu ulazima wa kuwasiliana na kushirikiana, ili kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa malalo hizo, hususan wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.