Majmaa-Ilmi imefanya semina za kuwajengea uwezo walimu wa Qur’ani katika mkoa wa Swalahu Dini.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabaru Abbasiyya imefanya semina ya kuwajengea uwezo walimu wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mkoa wa Swalahu Dini.

Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa.

Wakufunzi wa Maahadi wametoa mihadhara ya kueleza (mbinu za ufundishaji, mafundisho ya uislamu, nafasi ya elimu katika kujenga kizazi chema kinachofata mafundisho ya vizito viwili), ikiwa kama sehemu ya kujiandaa na semina za kiangazi zinazotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Semina imedumu kwa muda wa siku mbili na ilikuwa na washiriki (140) walimu wakiume na wakike kutoka wilaya na mitaa tofauti, ambako zitafanywa semina zinazotarajiwa kuwa na washiriki (3000).

Maahadi inaendesha semina za kuwajengea uwezo walimu wa Qur’ani katika mikoa ya (Misaan, Waasit, Diwaniyya, Najafu, Kirkuuk na Swalahu Dini), Maahadi inatarajia kupokea wanafunzi zaidi ya (30000) kwenye semina za majira ya kiangazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: