Idara ya Dini tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imetoa wito wa kuhudhuira kwenye mafundisho ya ibada ya Hijja.
Inafanywa semina hiyo kutokana na kukaribia kwa safari za kwenda katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu kufaya ibada ya Hijja.
Semina itajikita katika kurekebisha makosa ambayo mara nyingi hufanywa na mahujaji wakati wa ibada ya Hijja, pamona na mambo mengine.
Semina ni maalum kwa wanawake tu, itafanywa katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) kilichopo eneo la Mulhaq Barabara ya Hospitali ya Husseini siku ya Alkhamisi na Ijumaa tarehe (16 – 17) mwezi huu wa tano, saa tisa Alasiri.
Kwa maelezo zaidi piga namba za simu zifuatazo:
07602273078
07702911920