Kiongozi wa idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya amesema kuwa, Hema la mabinti wa Aqida awamu wa kumi na tisa linawashiriki 2500 kutoka mikoa tofauti ya Iraq.
Kiongozi wa idara bibi Bushra Kinani amesema “Kutokana na ukubwa wa mwitikio wa hema la (Mabinti wa Aqida), imelazimu kuwagawa washiriki kwenye hema tofauti, kwa kufuata jografia ya kila chuo, kila hema tumeweka wanafunzi (250)”.
Akaongeza kuwa “Kuna wakufunzi mahiri wanaosimamia ratiba za hema”.
Kinani akasema “Katika hema hizo wanafundishwa mambo mbalimbali ya kitamaduni na Fiqhi, sambamba na kufanya mashindano, michezo na vipindi vya mapumziko”.