Tawi la Atabatu Abbasiyya katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu jijini Tehran, limeweka kipengele cha (Barua kwa kaburi) kwa wadau wake.
Maonyesho yanafanywa kwa mara ya (35) yamepata mahudhurio makubwa ya taasisi za uchapaji na usambazaji kutoka sehemu tofauti za dunia, yanalenga kubadilishana uzowefu na kuimarisha mawasiliano baina yao.
Mjumbe wa kamati ya maonyesho katika Ataba tukufu Sayyid Haidari Twalibu Abdul-Ameer amesema “Tawi la Ataba tukufu limeweka kipengele cha (Barua kwa kaburi) kwa ajili ya kuweka mafungamano ya kiroho baina ya watu wanaotembelea maonyesho haya na mwezi wa familia (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kipengele hicho kinahusisha kutoa nafasi kwa watu wanaotembelea maonyesho na kuweka kwenye sanduku maalum, kisha zitapelekwa kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na watumishi wa malalo hiyo tukufu”.
Akaendelea kusema “Kipengele hiki kinafanana na kipengele cha (Barua kwa kaburi) kilichopo kwenye toghuti ya Atabatu Abbasiyya tukufu (Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa) wenye lugha tisa”.
Maonyesho ya sasa yanashuhudia vipengele tofauti, ikiwa ni pamoja na watu kujisajili katika ukurasa wa ziara kwaniaba, kuweka ukurasa wa kifarisi kwenye App ya Haqibatu Mu-umin, kuonyesha kitabu cha fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda katika tawi la Ataba tukufu.