Muheshimiwa akataja baadhi ya mazingatio ya jela anayoweza kunufaika nayo muumini, akasema “Jela huwa ni rehma na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo humpa muumini, kwani hupata nafasi nzuri ya kuwasiliana na mwenyezi Mungu mtukufu na hukatika mawasiliano na watu wengine wote, mwanaadamu huwa mbali na mitihani ya dunia ambayo huipata mtu asiyekua jela”.
Akasema kuwa “Miongoni mwa malezi ya Mwenyezi Mungu kwa mwanaadamu, ni kumfanya aishi katika hali ya kudhulumiwa na kupangiwa uhuru, ili ahisi machuni na kutambua rehema ya Mwenyezi Mungu katika Maisha yake, muumuni anapaswa kutumia jela kumuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu na kuhakikisha Maisha yake yote anaendelea kumtumikia Allah na kuacha historia njema ya kujitolea kwake”.
Akabainisha kuwa “Baadhi ya watu wanaweza kufeli katika Maisha ya dunia na kuwa madhalimu, baada ya Mwenyezi Mungu kumuondoa katika matatizo na kuona mabadiliko makubwa yaliyotokea baada ya mwaka 2003 kwa kuondolewa muovu”.
Wajibu wa mwanaadamu hapa duniani ni kufanya aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu na kushikamana na njia ya haki daima, haki haitambuliwi kwa kuangalia watu bali kwa kuangalia haki”.
Mfungwa wa kisiasa wa zamani na mmoja wa wajumbe hao Sayyid Maahir Hasani akasema “Leo tumemtembelea Muheshimiwa Sayyid Ahmadi swafi kutokana na wito wale kwetu, kundi la watu waliokuwa pamoja nae walikuja jela wakati wa utawala uliopita”.
Akaongeza kuwa “Ziara hii inatukumbusha kuwa hatuwezi kusahau miongo ya mateso tuliyopitia, tutaendelea kueleza kwa vizazi vijavyo dhulma tulizo fanyiwa na utawala wa Baathi, uli udikteta kama ule usirudi tena”.
Akaendelea kusema kuwa “Sayyid Swafi ameonyesha umuhimu wa kuandika kitabu cha (Wafungwa wa kisiasa) kama vile kitabu cha Mausua waafi litauthiiq wa dirasaati fil-Atabatu Abbasiyya, kitakacho Andika tuliyo shuhudia na kusikia miongoni mwa visa vya ushujaa na kujitolea kwa wale waliouawa katika njia hiyo”.
Akasema kuwa “Kuna umuhimu wa kuendelea kuwasiliana baina ya watu walionyanyaswa na utawala uliopita”.