Kongamano linasimamiwa na jumuiya ya Al-Ameed, ni sehemu ya wiki ya Imamu ya kimataifa awamu ya pili, yenye kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu vitu viwili visivyoachana) na anuani (Mwenendo wa Maimamu -a.s- katika malezi ya mtu na jamii) tarehe (25 Dhulhijja 1445h) sawa na (2 Julai 2024m).
Jumuiya imepokea mihtasari (20) na tafiti za kielimu (17) sambamba na maandiko kutoka nchi tofauti za kiarabu na kiislamu.
Mada za kongamano zinaendana na riwaya za Imamu Ridhwa (a.s), kuhusu maarifa ya Qur’ani, tafsiri, malezi, Aqida, Fiqhi, Sikolojia, jamii, maadili, utamaduni, afya na mazingira.