Watumishi wa idara wamezowea kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), likiwemo la kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s).
Kazi ya upambaji wa dirisha imehusisha kuweka mauwa yenye rangi tofauti na harufu nzuri, kwa lengo la kuongeza uzuri juu ya uzuri kwenye malalo ya mwezi wa bani Hashim (a.s).
Atabatu Abbasiyya huweka mapambo yanayoashiria furaha juu ya dirisha la kaburi takatifu katika kuadhimisha mazazi ya watakasifu miongoni mwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s).