Idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa zawadi za tabaruku kwa mazuwaru kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Ridhwa (a.s).
Kiongozi wa idara Sayyid Hashim Shaami amesema “Wahudumu wa idara ya Masayyid wametoa zawadi ya tabaruku kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Idara hutoa umuhimu mkubwa katika kuadhimisha matukio yote yanayohusu Ahlulbait (a.s) hususan malazi yao matukufu, hutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kujenga misingi ya Dini na utamaduni”.