Idara ya Majmaa-Afaaf ya wanawake chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, imetoa wito wa kushiriki kwenye maonyesho ya biashara ya kwanza ya wanawake.
Maonyesho yatafanywa kwenye uwanja wa kitua cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo (Tunafanya kazi ili tufanikiwe na kuendelea) siku ya Jumamosi ya tarehe (8/6/2024), yatakuwa na awamu mbili, ya kwanza kuanzia saa nne asubuhi hadi saa saba mchana, na saa kumi na moja na nusu hadi saa mbili ya nusu jioni.
Maonyesho yanalenga kujenga uwezo wa wanawake na kuwapa nafasi ya kununua bidhaa mbalimbali, jambo ambalo linaongeza Uchumi wao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu namna ya kushiriki kwenye maonyesho hayo na kanuni zake piga simu ifuatayo (07602466880) au wasiliana nasi kwa WhatsApp/ Telegram.