Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s) katika viwanja vya ukanda wa kijani.
Rais wa kitengo cha ukanda wa kijani chini ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Nasoro Hussein amesema “Miongoni mwa hafla za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuadhimisha tukio hili, ni hafla kubwa iliyofanywa katika viwanja vya ukanda wa kijani, kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehudhuriwa na familia za ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ilikuwa na washairi na waimbaji waliosoma mashairi na qaswida za kumsifu Imamu (a.s)”.
Akaendelea kusema “Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha mazazi ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kuelezea historia zao tukufu”.