Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) katika eneo la vitalu vya Alkafeel.
Kiongozi wa eneo hilo Sayyid Muhammad Harbi amesema “Hafla iliyofanywa katika eneo la vitalu vya Alkafeel imepambwa na qaswida, mashairi na tenzi sambamba na kugawa maua na zawadi za tabaruku kwa wahudhuriaji”.
Akaongeza kuwa “Hafla imepata mahudhurio makubwa ya familia za wakazi wa Karbala, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi kubwa ya kutoa mafundisho ya Ahlulbait (a.s) na mwenendo wao katika jamii kupitia matukio mbalimbali ya kidini”.