Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza utekelezaji wa mradi wa semina za Qur’ani za kiangazi katika mkoa wa Muthanna kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (3000).
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu/ tawi la Muthanna chini ya Majmaa Sayyid Muhammad Aali Bahiyya amesema “Maahadi imeanza utekelezaji wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi katika mkoa wa Muthanna kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (3000) wakiwa kwenye misikiti na Husseiniyya (75) hapa mkoani”.
Akaongeza kuwa “Wanafunzi wanafundishwa masomo ya Qur’ani, kusoma na kuhifadhi, Fiqhi, Aqida, Sira na Akhlaqi, kuna walimu (120) wanaofundisha kwa kufuata selebasi maalum inayo endana na aina ya wanafunzi walionao”.
Majmaa hufanya mradi huu kila mwaka kwenye mkoa wa Baghdad na mikoa mindine ya Iraq, kwa lengo la kunufaika na wakati wa likizo za kiangazi, kwa kuwajenga wanafunzi katika mafundisho ya Dini na maadili chini ya maelekezo ya vizito viwili.