Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, kimezindua kisima kipya katika mji wa Manakora nchini Madagaska kwa ajili ya kusambaza maji kwa maelfu ya familia.
Kisima kimepewa namba (29) kikiwa ni miongoni mwa visima vinavyo chimbwa kwenye nchi zaidi ya (13) barani Afrika, kupitia mradi wa (Saaqi Atwasha Karbala) unaotekelezwa na Atabatu Abbasiyya katika bara la Afrika, kisima hiki kimepewa jina la (Baabul-Hussein -a.s-).
Hafla ya uzinduzi wa kisima imehudhuriwa na viongozi wa mji na kundi la wakazi, wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa Markazi Dirasaati Afriqiyya, kwa kuwajali na kuwachimbia kisima.
Mradi wa (Saaqi Atwasha Karbala) umeanza kutekelezwa miaka kadhaa iliyopita katika bara la Afrika, kwa lengo la kuwasaidia katika sekta ya kilimo na kuzipatia maelfu ya familia maji safi na salama ya kutumia.