Kwa ushiriki wa walimu (400).. Wanafunzi wanaendelea na semina za Qur’ani katika mji wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha semina za Qur’ani za majira ya kiangazi katika mkoa wa Baabil kwa ushiriki wa wanafunzi elfu (10) chini ya ukufunzi wa walimu (400).

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya kitengo Sayyid Muntadhiru Almashaikhi amesema “Majmaa-Imi ya Qur’ani imeanza kutekeleza mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi, kwa ushiriki wa wanafunzi elfu (10), semina zinafanyika kwenye misikiti na Husseiniyya (300) chini ya wakufunzi (400)”.

Akaongeza kuwa “Walimu wa Maahadi sambamba na masomo ya Qur’ani wanafundisha Aqida, Fiqhi na historia ya Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kutengeneza kizazi kinachoshikamana na mafundisho ya Dini ya kiislamu na mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi Shekhe Jihadi Kaabi, ameushukuru uongozi wa Ataba tukufu kwa kutoa elimu bora kwa wanafunzi na kuwafundisha maadili ya Dini tukufu ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: