Kupitia maukibu ya kutoa huduma.. Atabatu Abbasiyya inahudumia misafara ya mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Maukibu ya Atabatu Abbasiyya tukufu inahudumia misafara ya mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Blugedia wa kikosi cha Abbasi (a.s) Saadi Maliki Hashim amesema “Kikosi kinasaidia kuweka ulinzi kwenye misafara ya mahujaji sambamba na kutoa huduma mbalimbali”.

Akaongeza kuwa “Huduma zinazotolewa ni pamoja na vituo vya afya, kwa ajili ya kupambana na dharura yeyote ya kiafya inayoweza kutokea kwa mahujaji, na ugawaji wa chakula na maji safi ya kunywa”.

Akafafanua kuwa “Ushiriki wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika kulinda misafara ya mahujaji unafanywa kwa kushirikiana na viongozi wa jeshi la serekali wa mkoa wa Karbala”.

Atabatu Abbasiyya imeandaa zaidi ya watumishi wake (1000) kuja kutoa huduma mbalimbali kwa mahujaji na kuimarisha ulinzi wa misafara yao, imekuwa ikifanya hivyo toka mwaka 2015m.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: