Majmaa-Ilmi imefanya hafla ya Arshu-Tilawah mbele ya wageni kutoka Waasit.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya Arshu-Tilawah ya usomaji wa Qur’ani wa kila wiki mbele ya wageni kutoka mkoa wa Waasit.

Mmoja wa watumishi wa mradi wa Qur’ani chini ya Majmaa Sayyid Thaamir Furtwausi amesema “Kituo kimeratibu usomaji wa Qur’ani kupitia ratiba ya kila wiki mbele ya wageni kutoka mkoa wa Waasit”.

Akaongeza kuwa “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanyika mwaka mzima, kila wiki hukaribisha wageni wapya kutoka katika mmoja wa mikoa ya Iraq”.

Akabainisha kuwa “Lengo la ratiba hii ni kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani tukufu katika malalo na kuwasiliana na taasisi za Qur’ani zilizopo kwenye mikoa tofauti ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: