Sayyid Swafi amepongeza shule za Al-Ameed kwa kuongoza kuwa na matokeo mazuri katika shule za Karbala.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amepongeza shule za Al-Ameed kwa kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya darasa la sita miongoni mwa shule za msingi za Karbala.

Pongezi hizo zimetolewa na rais wa kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu Dokta Abbasi Rashidi Didah Mussawi kwaniaba ya Sayyid Swafi.

Shule za Al-Ameed zimeongoza kwa kuwa na matokeo mazuri katika shule za Karbala kwenye mitihani ya wizara ya darasa la sita mwaka 2023 – 2024m, shule za Al-Ameed zimeshinda kwa kiwango cha juu kama ifuatavyo:

Shule ya msingi Al-Ameed ya wasichana % 100.

Shule ya msingi Alqamaru ya wasichana % 100.

Shule ya msingi Nurul-Abbasi ya wasichana % 100.

Shule ya msingi Al-Ameed ya wavulana % 100.

Shule ya msingi Nurul-Ameed ya wavulana % 100.

Shule ya msingi Nurul-Abbasi ya wavulana % 92.

Mussawi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa shule hizo baada ya kukutana nao, iliyopelekea kupata ufaulu mkubwa, aidha amewapongeza wanafunzi kwa ufaulu huo.

Ametoa pongezi pia kwa wazazi wa wanafunzi kwa kufatilia maendeleo ya Watoto wao na kuwasimamia vizuri katika masomo yao na kutoka ushirikiano mkubwa kwa viongozi wa shule, akawatakia walimu wakuu, wasaidizi wao, walimu wa masomo na wanafunzi wote mafanikio mema. Akasisitiza ufaulu huu unaonyesha uwajibikaji wa kiwango cha juu wa viongozi wa shule na uwepo wa mazingira mazuri ya ufundishaji na usomaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: