Kitengo cha habari kinafanya semina ya kuwajengea uwezo watumishi.

Kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina ya kuwajengea uwezo baadhi ya watumishi.

Semina hiyo imesimamiwa na kituo cha mafunzo ya Habari chini ya kitengo.

Mkufunzi Sayyid Yaasir Karim amesema “Semina za kuwajengea uwezo watumishi hufanywa kwa siku tano (5), huwa zinamada kuu tatu ambazo ni, majukumu kabla ya kazi, wakati wa kazi na baada ya kazi, mambo gani anatakiwa kuyajua muandaaji wa kipindi katika maswala ya picha, sauti na mengineyo”.

Akaongeza kuwa “Semina ilikuwa na masomo ya nadhariya na vitendo, kila muhadhara ulidumu kwa muda wasaa mbili, aidha washiriki wamepewa nafasi ya kuuliza maswali na kupewa ufafanuzi zaidi”.

Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya semina na warsha za kuwajengea uwezo watumishi wake katika sekta tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: