Amesema kuwa “Chuo kimeweka mazingira mazuri ya kufanya mitihani ya mwisho wa mwaka (2023 – 2024) kwa wanafunzi wake”.
Akaongeza kuwa “Mitihani ya mwisho wa mwaka ya wanafunzi wa chuo hufanywa kwa utaratibu mzuri chini ya kanuni zinazowekwa na kamati ya mitihani” akasisitiza kuwa “Maandalizi ya mitihani hutakiwa kukidhi vigezo vya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu”.
Akaendelea kusema “Kamati ya mitihani ya chuo inafanya kazi pamoja na kamati ya wizara inayohakikisha taratibu zote zilizowekwa na wizara zinafatwa kikamilifu kwenye mitihani hiyo”.