Kituo cha utamaduni wa familia kinashiriki kwenye semina ya Yanabia-Rahmah.

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kinashiriki kwenye semina ya (Yanabia-Rahmah).

Mkuu wa kituo bibi Sara Hafaar amesema “Kituo kinaendelea kushiriki katika semina ya (Yanabia-Rahmah) inayosimamiwa na idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) kwa lengo la kutoa mafunzo ya kitamaduni na kijamii kwa mabinti”.

Akaongeza kuwa “Semina ni maalum kwa mabinti wenye umri wa miaka sita (6) hadi kumi na sita (16), muhadhara wa semina umepewa anuani isemayo (Fikra Chanya), umetolewa na Imani Auni, amefafanua uzowefu wa matendo yanayotokana na fikra hasi katika maisha ya mwanaadamu, na namnagani unaweza kubadilisha fikra hasi kuwa Chanya”.

Akabainisha kuwa “Muhadhara ulukuwa na sehemu mbili, sehemu ya kwanza kumbukumbu ya chuma, ya pili kuvunja ugumu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: