Muheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, amempokea kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Shekhe Abdulmahadi Karbalai na amepongeza juhudi yake kwenye sekta tofauti, hususan sekta ya afya.
Tamko la ofisi ya Marjaa Dini mkuu linasema “Sayyid Sistani amempokea muwakilishi wake na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Shehe Abdulmahadi Karbalai, na amepongeza juhudi kubwa anayofanya kwenye sekta tofauti, hususan sekta ya afya”.
Tamko limebainisha kuwa “Marjaa Dini mkuu amebariki uzinduzi wa miradi tofauti uliofanywa hivi karibuni katika mkoa wa Basra, amemshukuru kwa hilo na kumuombea mafanikio zaidi”.