Sayyid Swafi amekagua ratiba ya semina za kiangazi kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekagua ratiba ya semina za majira ya kiangazi kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed.

Amefanya hivyo alipotembelea uongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, amepokewa na rais wa kitengo hicho Dokta Hassan Daakhil Karim.

Kiongozi mkuu wa kisheria amepewa maelezo ya ratiba ya semina za majira ya kiangazi iliyoandaliwa na viongozi wa shule za Al-Ameed kwa makundi tofauti ya wanafunzi.

Sayyid Swafi amempongeza rais wa kitengo hicho kwa ufaulu mzuri wa shule za Al-Ameed (za wavulana na wasichana) kwenye mitihani ya wizara ya darasa la sita mwaka huu (2023 – 2024m), akasema kuwa ufaulu huo unatokana na kazi nzuri iliyofanywa na watumishi na walimu wa shule, pamoja na changamoto nyingi walizonazo.

Akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya ikotayali kusaidia mradi huo ili uweze kufikia malengo yake na kufanikisha ndoto za wazazi na wadau wa shule, kwani wao ni washiriki wa matokeo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: