Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia kundi kubwa la waumini walioshiriki usomaji wa Dua-Nudba asubuhi ya Ijumaa.
Msomaji Sayyid Ali Mamitha amesema “Asubuhi ya kila Ijumaa husomwa Dua-Nudba ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ushiriki wa kundi kubwa la mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameweka vitabu vingi vya dua kwa ajili ya mazuwaru, sambamba na kusafisha haram tukufu”.
Akabainisha kuwa “Dua imesomwa katika mazingira tulivu ya kiibada”.