Semina za Qur’ani za majira ya kiangazi zinazofanywa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, zimepata muitikio mkubwa katika wilaya ya Ainu-Tamru.
Semina hizo zinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (616) waliosambazwa katika misikiti na husseiniyya (22) chini ya walimu (22).
Semina zinaratiba tofauti, kuna usomaji wa Qur’ani, mashindano, masomo ya nadharia na vitendo, Fiqhi, Aqida, Akhlaq na Sira.
Semina hizo zinalenga kujenga uwelewa wa mafundisho ya Dini na utamaduni kwa vijana sambamba na kuandaa jamii ya watu wenye maadili mema.